John 21:1-11

Yesu Awatokea Wanafunzi Saba

1 aBaada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia.
Yaani Bahari ya Galilaya.
Yeye alijionyesha kwao hivi:
2 cSimoni Petro, Tomaso aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3 dSimoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.

4 eMara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu.

5 fYesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?”

Wakamjibu, “La.”

6 gAkawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.

7 hYule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini. 8Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200
Dhiraa 200 ni kama mita 90.
9 jWalipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.

10Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.”

11Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Copyright information for SwhNEN